Genesis 7

1 aNdipo Bwana akamwambia Nuhu, “Ingia katika safina wewe na jamaa yako yote, kwa sababu katika kizazi hiki nimeona ya kuwa wewe ni mwenye haki. 2 bUchukue wanyama saba walio safi wa kila aina, wa kiume na wa kike, na wanyama wawili wawili wa kila aina walio najisi wa kiume na wa kike. 3 cPia uchukue ndege saba walio safi wa kila aina, wa kiume na wa kike, ili kuhifadhi aina zao mbalimbali katika dunia yote. 4 dSiku saba kuanzia sasa nitaleta mvua juu ya nchi kwa siku arobaini usiku na mchana, nami nitafutilia mbali kutoka uso wa nchi kila kiumbe hai nilichokiumba.”

5 eNuhu akafanya yote kama Bwana alivyomwamuru.

6 fNuhu alikuwa na miaka 600 gharika ilipokuja juu ya dunia. 7 gNuhu na mkewe na wanawe na wake zao wakaingia katika safina ili waepuke ile gharika. 8Jozi ya wanyama walio safi na walio najisi, ndege na viumbe vitambaavyo, 9 hwa kiume na wa kike, walikuja kwa Nuhu wakaingia katika safina kama Mungu alivyomwamuru Nuhu. 10Baada ya siku saba, maji ya gharika yakaja juu ya dunia.

11 iKatika siku ya kumi na saba ya mwezi wa pili mwaka wa 600 wa kuishi kwake Nuhu, siku hiyo ndipo chemchemi zote hata zilizo chini sana ya ardhi zilibubujika kwa nguvu, na malango ya mafuriko ya mbinguni yakafunguliwa. 12 jMvua ikanyesha juu ya nchi siku arobaini usiku na mchana.

13 kSiku hiyo Nuhu, na mkewe, na wanawe Shemu, Hamu na Yafethi pamoja na wake zao wakaingia katika ile safina. 14 lNao walikuwa pamoja na kila mnyama wa mwituni kufuatana na aina yake, wanyama wote wafugwao kufuatana na aina zao, kila kiumbe kitambaacho juu ya ardhi kwa aina yake, na kila ndege kufuatana na aina yake, naam kila kiumbe chenye mabawa. 15 mViumbe vyote vyenye pumzi ya uhai ndani yake vikaja kwa Nuhu viwili viwili, vikaingia katika safina. 16 nWanyama walioingia katika safina walikuwa wa kiume na wa kike, wa kila kiumbe chenye uhai kama Mungu alivyomwamuru Nuhu, ndipo Bwana akamfungia ndani.

17Kwa siku arobaini mafuriko yaliendelea kujaa duniani na maji yalivyozidi kuongezeka, yaliinua safina juu sana kutoka kwenye uso wa nchi. 18Maji yakajaa na kuongezeka sana juu ya nchi, na safina ikaelea juu ya uso wa maji. 19 oMaji yakazidi kujaa juu ya nchi, yakaifunika milima yote mirefu chini ya mbingu yote. 20 pMaji yakaendelea kujaa yakaifunika milima kwa kina cha zaidi ya dhiraa kumi na tano.
Dhiraa 15 ni sawa na mita 7.
21 rKila kiumbe hai kitambaacho juu ya nchi kikaangamia: Ndege, wanyama wa kufugwa, wanyama pori, viumbe vyote juu ya nchi na wanadamu wote. 22 sKila kiumbe juu ya nchi kavu chenye pumzi ya uhai kikafa. 23 tKila kitu chenye uhai juu ya uso wa nchi kilifutiliwa mbali, watu, wanyama, viumbe vitambaavyo na ndege warukao angani wakafutiliwa mbali toka duniani. Waliobaki ni Nuhu peke yake na wale waliokuwa pamoja naye ndani ya safina.

24 uMaji yakaifunika dunia kwa siku 150.
Copyright information for SwhKC